2010年4月20日火曜日

Sababu/Reason

Shikamooni mabibi na mabwana.
Habari zenu rafiki zangu?

Siku hizi hari ya hewa ya okinawa hapa ninapokaa
inabadirika kila siku.
Jana kulikuwa na joto sana, lakini leo kuna mvua na baridi.
Kwa hiyo kila asubuhi ninaangaika "leo ninavaa nguo gani?".

Leo napenda kuwaanbia kwa nini ninaandika blog kwa kiswahili.

kwa sababu...

Mwaka ya 2007, nilienda Tanzania kwa volunteer.
Nilifanya kazi ya UKIMWI katika manispaa
pamoja na maofisa ya manispaa na watu wa asasi.
Nilikaa miaka miwili kwenye jamii ya uswahilini.
Nilienda kazi asubuhi na nilitembea mahali mbalimbali siku nzima.
Nilikaa mjapani mmoja yaani mimi tu katika kata hiyo.
Kwa hiyo nilijifunza kiswahili, na nilipata lugha hiyo kidogo kidogo.

Kiswahili ni siyo gumu sana kwa kutamuka.
Na ninapenda watanzania, nilitaka kuwasiliana nao.

Hivyo...

Mpaka sasa nipo Japani, naweza kutumia kiswahili.
Ila nimeshaanza kusahau kidogo kidogo, kwa hiyo natumia kwenye blog hii.


Napenda kukupendekeza upate lugha hiyo!
Utaweza kuongea na watanzania na mimi :-)

0 件のコメント:

コメントを投稿